Na. Faraja
Gasto
Utangulizi
Kuna umishenari unaohusisha mtu mmoja (Mwanzo
6:13-22)(Yona 1:1-2) na kuna umishenari unaohusisha kundi la watu kadhaa
(Nehemia 4:13-14). Ukisoma maandiko hayo utaona umishenari ukitajwa hapo.
Somo hili ni
kwa ajili ya watu wote wenye maono ya kuwa mishenari watakaoongoza makundi
katika kufanya umishenari katika maeneo mbalimbali.
à Kila
mishenari anatakiwa kuyajua mambo haya ya msingi kuhusu umishenari, katika somo
hili tutajifunza mambo kadhaa kuhusu umishenari kutoka kwa Bwana wetu Yesu
Kristo.
Mambo ya
msingi ambayo kila mishenari anatakiwa kuyafahamu
1.Tafuta watu unaotaka kufanya nao kazi
unayokusudia kuifanya.
(Mathayo
4:18-21)
à Yesu
aliwafuata watu aliotaka kufanya nao kazi , kwa hiyo unapokuwa mishenari lazima
uwatafute watu unaotaka kuwa nao, Yesu hakufanya maombi ya kuwavuta waje bali
alipotoka kwenye maombi alianza kuwafuata watu ambao anawataka.
2.Waambie aina ya kazi wanayokwenda kuifanya.
(Mathayo
4:18-19)
à Yesu
aliwaambia wamfuate kwa kuwa anataka kuwafanya kuwa “wavuvi wa watu” kwa hiyo
Yesu alipowatafuta watu aliotaka kufanya nao kazi aliwaambia aina ya kazi
ambayo anataka waifanye.
3.Waandae kwa ajili ya kazi iliyoko mbele
yao.
(Mathayo
4:18-19)
à Yesu
alipowatafuta watu anaotaka kuwa nao na akawaambia aina ya kazi anayotaka
waifanye, Yesu alianza kuwaandaa kwa ajili ya kazi iliyoko mbele yao ndio maana
Yesu aliwaambia “NITAWAFANYA” neno hilo kuwafanya maana yake ni
kuwaandaa/kuwatengeneza kwa ajili ya kazi iliyoko mbele yao. Wanafunzi wa Yesu
walikuwa hawajui maana ya kuwa “wavuvi wa watu” ni nini na watu wanavuliwaje,
kwa hiyo ilimpasa Yesu awaandae kwanza, kuwaandaa kulihusisha kuwapa uelewa wa
kutosha juu ya ile kazi na namna ya kuifanya.
Kwa mfano kama unataka kuanzisha kundi
linalokusudia kupambana na rushwa, lazima kwanza wanakikundi wajue rushwa ni
nini, madhara ya rushwa ni yapi, faida za kutopokea rushwa ni zipi n.k.
4.Usiwe na watu wa aina moja katika kundi.
(Mathayo
4:18-22)
à Yesu alikuwa
na wanafunzi waliokuwa wakijishughulisha na mambo mbalimbali kwa mfano Mathayo
na Lawi walikuwa watoza ushuru (Marko 2:14)(Mathayo 9:9). Petro, Andrea na
wengine walikuwa wavuvi (Mathayo 4:18-22).
Unapokuwa na watu wa aina tofautitofauti
inalifanya kundi kuwa na watu wenye uwezo wa kufanya kazi mbalimbali.
Tunajifunza kwa Mfalme Sulemani alipokuwa
akitaka kujenga hekalu, alitafuta watu wenye ujuzi mbalimbali; wataalamu wa
kuchora, kuchonga, kujenga n.k.
5.Wape nafasi ya kutendea kazi kile
unachotaka wakifanye (usifanye peke yako)
(Luka
10:117-20)
Yesu hakuishia
kuwaanda/kuwafundisha bali aliwapa nafasi ya kutendea kazi kile ambacho
aliwafundisha, aliwaacha waende kule alikokuwa anataka yeye aende, hiyo yote
ilikuwa ni kuwapa nafasi watendee kazi kile alichowafundisha na waliporudi
walileta ripoti ya kazi waliyokwenda kufanya.
6.Waamini watu unafanya nao kazi.
(Luka 10:1)
Yesu aliwapa
wanafunzi wake jukumu ambalo alitakiwa kulifanya yeye mwenyewe, tunachojifunza
kwa Yesu ni kwamba alipowafundisha wanafunzi wake aliwaamini kuwa wanaweza
kufanya kile alichowafundisha ndio maana aliwapa nafasi ya kutekeleza majukumu
aliyotakiwa kuyatekeleza.
7.Lazima ufikiri kuhusu mahitaji ya kimwili
ya watu unaofanya nao kazi(maisha yao ya kila siku)
(Mathayo
17:24-27)
Kumbuka watu
unaofanya nao kazi ni wanadamu kama wewe na wana mahitaji yao ya kila siku, kwa
hiyo unapokuwa mishenari unayeongoza kundi lazima ufikiri kuhusu maisha ya
watu(usitawi) unaofanya nao kazi.
Petro alipokuwa anadaiwa kodi alienda kwa
Yesu, Yesu akampa mbinu ya kupata fedha za kutatua tatizo alilokuwa nalo. Yesu
hakumpa Petro majibu ya matumaini bali Yesu alimpa Petro mbinu ya kupata fedha.
8.Waonyeshe faida watakayopata wanapofanya
kazi hiyo.
(Mathayo
19:27-29)
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake kuwa faida watakayopata katika kufanya kazi anayotaka
waifanye ni kwamba watapata mara mia katika ulimwengu huu na katika ulimwengu
ujao watapata uzima wa milele. Tunachojifunza hapo ni kwamba watu unaofanya nao
kazi wanapojua faida ya kazi ambayo wanaifanya watakuwa na hamasa(motivation)
ya kufanya hiyo kazi.
0 Maoni