Watu wengi wanapopitia shida au changamoto
mbalimbali hujikuta wamepoteza imani kwa Mungu jambo ambalo huwa linapelekea
waanze kuwategemea wanadamu kuliko Mungu na hata kutafuta msaada nje ya Mungu.
Nataka nikuonyeshe umuhimu wa kukumbuka
matendo makuu ya Mungu kwa kukupatia mifano kadhaa iliyomo kwenye Biblia.
1.Daudi (1
Samweli 17;23-24, 31-37)
Wakati ambapo Goliathi aliinuka na kuwatukana
wana wa Israeli tunaona hakuna mtu aliyethubutu kwenda kupigana na Goliathi
lakini Daudi aliposikia hayo matusi ilimuumiza sana na ilipomuumiza alikwenda
kwa Mfalme Sauli na kumwambia kuwa mimi nitakwenda kupigana na Goliathi na
kumuua, kumbuka Daudi anayasema hayo lakini yeye si mwanajeshi, maneno yake
yaliposikiwa na Mfalme, Mfalme alimwambia huwezi kupgana na huyo jamaa kwa kuwa
yeye ni mtu wa vita tangu ujana wake lakini Daudi akamwambia Mfalme kuwa “kama
Mungu aliniokoa na makucha ya simba na dubu” basi huyu mfilisti nitamuua pia.
Daudi alikumbuka matendo makuu ya Mungu na ndio maana akapata uajasiri wa
kukabiliana na Goliathi.
2.Nabii
Eliya (1 Wafalme 18;22-24)
Nabii Eliya alipowaambia watu waje washuhudie
nani ni Mungu wa kweli kati ya Baali na Bwana kwa kuwaambia kuwa Mungu
atakayejibu kwa moto ndiye Mungu wa kweli Biblia haituambii kuwa Eliya amewahi
kuomba na moto ukashuka, ila Nabii Eliya alikumbuka kuwa kama amewahi kuomba
mambo makubwa na Mungu akafanya basi hata siku hiyo Mungu atashusha moto na
ndio maana Nabii Eliya hakuwa na mashaka na Mungu wake.
à Wana wa
Israeli walipta matatizo makubwa sana kwa kuwa walikuwa wasahaulifu wa matedno
makuu ya Mungu, hawakukumbuka mambo makubwa ambayo wamewahi kuyaona kwa macho
Mungu akifanya ndio maana walipokumbana na changamoto waliacha kumuamini Mungu
na mwishowe wakaangamia, kama wangekuwa watu wa kukumbuka kuwa kama Mungu
aligawanya Bahari na wakapata njia, kama kuta za Yeriko zilianguka, kama mwamba
ulitoa maji n.k basi ilikuwa ni sababu tosha ya kuwafanya wasiwe na hofu na
Mungu wao lakini kwa kwa kuwa walisahau matendo makuu ya Mungu ndio maana
waliangamia.
3.Uuumbaji
wa Mungu (Zaburi 24:1)
Ikiwa unatambua Mungu ndiye aliyeumba kila
kitu, basi hiyo ni sababu tosha ya kukufanya uzidi kuweka imani yako kwa Mungu,
kwa kuwa hakuna jambo gumu lolote asiloliweza Bwana.
ANGALIZO: Unapokumbana na tatizo usiangalie
tatizo hebu angalia na ukumbuke matendo makuu ya Mungu aliyowahi kuyafanya na
kisha angalia tatizo ulilonalo je! vinalingana? Na kama havilingani basi una
sababu tosha ya kukufanya uzidi kumwamini Mungu, ikiwa Mungu alifufua wafu
hajashindwa kukuponya ugonjwa, ikiwa alitoa maji kwenye mwamba hajashindwa
kufanya chochote unachoomba n.k.
Mungu akubariki kwa kujifunza.
Kwa nini ukumbuke matendo makuu ya Mungu?
1.Itakusaidia kuimarisha imani yako kwa Mungu kwa kuwa pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu (waebrania 11:6)
2.Itakusaidia kutengeneza ujasiri ndani yako wa kukabiliana na tatizo
(1 Samweli 17;23-24, 31-37)
(1 Samweli 17;23-24, 31-37)
Kwa
ushauri/maswali n.k usisite kuwasiliana nami
0767955334
1 Maoni
Amen
JibuFuta