FARAJA GASTO
Je! imefikia hatua umeona hakuna umuhimu wa
kuendelea kuishi(unatamani kufa au kujiua)?
Ni vema ujue shida iko kwenye NAFSI YAKO
kumbuka “aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo” (Mithali 23:7a))
Ni vema ujue tatizo la kupoteza furaha(hamu)
ya kuendelea kuishi halijaanza leo, limeanza zamani sana na ninataka nikupe
mifano ya watu wachache kwenye Biblia waliopoteza furaha ya kuendelea kuishi na
nini kilichotokea.
1.Nabii Eliya (1 Wafalme 19: 1-17)
Ukisoma hiyo habari utaona ni wakati ambapo
Eliya alikuwa amemaliza kuwaangamiza manabii wa Baali na taarifa ilipomfikia
Yezebeli(mke wa mfalme), Yezebeli akaapa lazima amuue Nabii Eliya, kwa hiyo
Nabii Eliya aliposikia hiyo taarifa akakimbia huku anaomba AFE, maana yake ni
kwamba alikuwa amekata tama(amepoteza furaha ya kuendelea kuishi) lakini
ulikuwa si wakati sahihi wa Eliya kuondoka duniani ila kwa kuwa alikuwa
amechoka aliomba AFE.
2.Yuda Iskariote (Matendo ya mitume 1:15-18)
Yuda baada ya kumsaliti Yesu, Yuda alijisikia
hatia kubwa moyoni mwake hivyo basi akaamua kujiua kwa sababu aliona haina haja
ya uendelea kuishi ndio maana akajiua.
à Hapa
nizungumze na vijana wa kike, mabinti wengine wamejikuta wakipoteza furaha ya
kuendelea kuishi kwa sababu ya hatia zilizomo moyoni kulingana na makosa
waliyoyafanya kama vile kutoa mimba n.k hata lakini haina haja ya kuwaza kufa
wakati Yesu anayesamehe Yupo.
Mambo kadhaa
yanayopoteza furaha(hamu) ya kuendelea kuishi
1.Kukata tama
2.Ugumu wa maisha
3.Magonjwa
Mambo ya
kufanya ili uzidi kuwa na furaha(hamu) ya kuendelea kuishi
1.Mpe Yesu
maisha yako (kama haujaokoka)
Kwa nini uokoke? Ni kwa sababu kazi mojawapo
ya Yesu ni kumpa mtu pumziko pale linapokuja jambo la kumlemea (Mathayo 11:28)
kwa kuwa moyo unapolemewa na mambo magumu ni rahisi mtu kujikuta umekata tamaa
ya kuendelea kuishi lakini unapokuwa na Yesu na ukajifunza kwake “utapata raha
nafsini mwako”.
2.Linda moyo
wako (Mithali 4:23)
Jukumu la kulinda moyo wako si jukumu la
Mungu bali ni jukumu lako wewe mwenye moyo, kama huwa unasikia mtu akisema
“nimevunjwa moyo” maana yake ni kwamba amepata shida kwenye moyo, kwa hiyo kama
atadumu katika hali ya kuvunjika moyo ni rahisi sana kukitaka kifo, jaribu
kufikiri mtu ambaye amepatwa magonjwa mazito na ndugu,jamaa, familia n.k
wamemkimbia, ni rahisi sana mtu huyo kufa kwa kuwa moyo una shida.
à Zipo njia
kadhaa za kibiblia za jinsi ya kuulinda moyo, lakini nitazungumzia njia moja
ambayo ni “KUWA NA NENO LA MUNGU MOYONI MWAKO” kumbuka neno ni upanga, neno ni
nyundo n.k kwa hiyo ukiwa na neno la Mungu litakutia nguvu na kukupa ujasiri wa
kukabiliana na tatizo hata kama ni kubwa kiasi gani, neno litakupa furaha ya
kutosha, neno liakuongoza namna ya kuomba na unapoomba unapata matokeo makubwa
sana kumbuka Mungu analiangalia neno lake ili alitimize (Yeremia 1:12).
3.Usiuangalie
ukubwa wa tatizo bali angalia ukuu wa Mungu (Hesabu 13:31-33)
Wapelelezi walirudi na habari mbaya za
kuvunja mioyo kwa kuwa walipotazama mambo mbalimbali ghafla wakaanza kuangalia
kile kilicho mbele yao badala ya kuangalia ukuu wa Mungu wao mwishowe ndani yao
iliingia HOFU, imani ikatoweka ndani yao na imani ilipotoweka ndani yao NAFSI
zao zikapata shida, wakaanza kujiona kama MAPANZI(grasshoppers).
à Watu wengi
wamejikuta wakipoteza furaha ya kuendelea kuishi kwa sababu ya Hofu inayotokana
na mazigira Fulani; hofu ya ugumu wa maisha, hofu ya kufa n.k, kilichomfanya
Nabii Eliya akaanza kuomba AFE ni kwa sababu ya HOFU kwa kuwa alimuogopa
Yezebeli.
(Zaburi
46:1-2)
Daudi aliishinda hofu ya ugumu wa maisha kwa
kuwa alimwamini Mungu aliyemtegemea, ndio maana anasema “Mungu kwetu sisi ni
kimbilio na nguvu HATUTAOGOPA IJAPOBADILIKA NCHI”. Watu wengi hukata tama
kutokana na ugumu wa maisha na wengine imefikia hatua wanatamani ni bora wafe,
nikamsikia mama mmoja akisema kwa hali hii ni bora mtu anakufa tu, ni kweli
huyo mama alikuwa anapitia matatizo kama ya kukimbiwa na mume wake na akaachwa
na watoto na pia alikuwa amechukua mkopo na anahangaika kurejesha, lakini swali
linakuja je! suluhisho ni kufa? Jibu ni
kwamba suluhisho sio kufa kwa kwa kuwa mtu akifa nje ya Bwana anakuwa amepata
hasara ya maisha yake yote, ni vema kujifunza kwa Daudi, tumfanye Mungu awe
kimbilio letu, huyo mama alikuwa anapitia hayo matatizo yote lakini hakuwa
karibu na Mungu (anaataka ajipiganie) na hiyo ni hatari sana, ukijaribu
kujipigania mwisho wake utajikuta umeumia na utapoteza hata hamu ya kuendelea
kuishi.
Mungu akubariki kwa kujifunza.
Kwa
ushauri/maswali n.k usisite kuwasiliana nami
0767955334
0 Maoni