Faraja Gasto
Utangulizi
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo
lipitalo majina yote.
Watu wengi wamejikuta wakitoka mahali
walipokuwa awali; kroho na kimwili. Ninapozungumzia kiroho namaanisha zamani
mtu alikuwa na uwezo wa kufunga na kuomba, kuamka usiku na kuomba, kutoa sadaka
nyingi n.k, kwa upande wa kiwmili namaanisha zamani mtu alikuwa na hali Fulani
kiuchumi, kiafya n.k lakini kwa sasa hana hali hiyo na anatamani kurudi angalau
mahali alipokuwa zamani na hajui anarudi vipi, hao ndio watu nataka kuzungumza
nao na kupitia somo hili watapata mbinu za kibiblia za kuwarudisha mahali
walipokuwa zamani.
Wengine kwa kwa kutojua mbinu zitakazowasaidia
kurudi walipokuwa zamani wamejikuta wakiwa katika hali ya kukata tamaa na
wengine wamejikuta wamepoteza furaha ya kuendelea kuishi kwa kuwaza kufa au
kujiua.
Mambo ya
kufanya ili kurudi ulipokuwa zamani
1.Kumbuka ni
wapi ulipokosea na kisha omba Toba na anza kufanya uliyokuwa unafanya mwanzoni (Ufunuo wa Yohana 2:5)
Ukisoma hiyo habari utaona kuna mambo ambayo
huyo mtumishi alikuwa akiyafanya kwanza lakini
ukafika wakati akaacha na alipoacha kumbe hakujua ANGUKO liko karibu ndio maana
analetewa ujumbe AKUMBUKE ni wapi ALIKOANGUKIA ATUBU na kisha aanze kufanya
alichokuwa anafanya mwanzoni ndipo ataweza kurudi kwenye NAFASI aliyokuwa nayo
mwanzoni.
à Jaribu
kufikiri mtu alikuwa mwombaji lakini ikafika hatua akatoka kwenye vile viwango
vya maombi maana yake ni kwamba ameanguka(ametoka katika NAFASI) aliyokuwa nayo
awali kwa hiyo ili arudi kwenye ile NAFASI lazima afanye mambo aliyokuwa
akifanya hapo awali.
à Kama mtu ni
mfanya biashara na imefikia hatua anapata hasara, lazima akumbuke zamani alifanyaje
na akapata faida na alikosea wapi, baada ya kukumbuka achukue hatua ya kufanya
alichokuwa anafanya mwanzoni.
(Luka
15:11-24)
Mwana mpotevu alipoteza FURSA ya kuishi
maisha ya furaha kwa kuwa alijitenga na nyumba ya baba yake mwishowe alijikuta
amekuwa ombaomba na akaanza kuwaza atawezaje kuishi maisha ya furaha kama
mwanzo? Baada ya tafakari hiyo ndipo AKAKUMBUKA kuwa kule kwao hakuna shida,
bali watu wanakula na kusaza ndipo akaamua kuchukua hatua ya KUTUBU na
alipotubu ndipo alijikuta amerudi kwenye NAFASI aliyokuwa nayo mwanzo.
à Hapa nataka
nizungumze na watu ambao hawajamwamini Yesu, jaribu kufikiri mtu amepata ukimwi
kwa sababu ya uzinzi au uasherati na afya yake imeharibika na anahitaji kuwa na
afya aliyokuwa nayo mwanzo, jaribu kufikiri mtu alikuwa tajiri na sasa utajiri
umekwisha na anahitaji kurudi kwenye hali nzuri ya uchumi kama mwanzo, kama
huyu mtu hana Yesu atajikuta anaangamiza familia yake au watu wengine ili apate
hali nzuri ya kiuchumi lakini ni vema kila mtu afajamu kuwa utajiri unaopatikana
kwa njia haramu huwa haudumu na huwa unamwangamiza aliyenao, lakini utajiri
unaopatikana kwa Mungu hauna huzuni ndani yake kwa kuwa Mungu ndiye anatupa
nguvu za kupata utajiri, kwa hiyo kama haujamwaminini Yesu mwamini sasa kwa
kuwa anaweza kukurudishia yale uliyopoteza atakusamehe maovu yote na atakuponya
magonjwa yote na atakupa afya njema (Zaburi 103:3).
2.Vaa silaha
zote za Mungu uweze kuzipinga hila za shetani (Waefeso 6:11)
Ni muhimu usimame katika maombi na kuweka
maarifa ya neno la Mungu ndani yako kwa kuwa shetani anataka kuona mtu akiwa
anapoteza nafasi(fursa) kila wakati kwa hiyo huwa na yeye anajipanga
kumshambulia mtu ili amtoe kwenye nafasi aliyopo kwa hiyo lazima mtu azivae
silaha zote za Mungu ili aweze kumshinda shetani.
Nataka nikupe mfano huu ili uweze kunielewa
vizuri.
(Danieli 6:4-28)
Watu waliinua fitina dhidi ya Danieli kama
ambavyo watu wanavyoinua fitina dhidi yaw engine ili wafukuzwe kazi n.k baada
ya hao watu kumuinukia Danieli wakatengeneza mpango makakati ili Danieli aondolewe
kwenye NAFASI aliyokuwa nayo kwanza, kumbuka ile nafasi aliyokuwa nayo
ilimfanya aishi vizuri(alikula mema ya nchi) na watumishi wenzake wakamuonea
wivu wakajipanga ili kumpoteza, lakini Danieli alikuwa mwombaji na hata
alipotupwa kwenye tundu la simba ili auawe, Mungu alimtuma malaika ili kuzuia
madhara yaliyokusudiwa dhidi yake.
à Danieli
alipoteza NAFASI ya uongozi kwa muda lakini kwa kuwa alizidi kumtumaini Mungu,
siku moja alirudishwa kwenye nafasi tena na waliomtakia mabaya wakauawa.
Mungu akubariki kwa kujifunza.
Kwa
ushauri/maswali n.k usisite kuwasiliana nami
0767955334
0 Maoni