NAFASI YA MAOMBI KATIKA KUSABABISHA WATU WAOKOLEWE


  

(Luka 10:1-2)

Yesu aliweka wazi kuwa mavuno ni mengi (watu walio tayari kuokoka ni wengi) lakini watenda kazi ni wachache wa kuvuna hayo mavuno.

Yesu alisema suluhisho la uchache wa watenda kazi ni maombi, tunapomwomba Bwana wa mavuno yeye anapeleka watenda kazi wakavune.

Maombi ndio yanasababisha Bwana wa mavuno kutuma watenda kazi wakavune mavuno ambayo ni mengi.

Kwa hiyo maombi yana nafasi ya kusababisha watu kuokolewa.

Kumbuka kuwa Biblia inasema "watu hawawezi kuamini bila kusikia mahubiri, na wahubiri hawawezi kwenda wasipopelekwa" rejea (Warumi 10:14-17).

HITIMISHO 

Tusiache kuomba, tuendelee kuomba ili Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi wakavune mavuno.

Chapisha Maoni

0 Maoni