(Isaya 41:21)
Watu wengi wanamuomba
Mungu lakini ni watu wachache wanaopeleka hoja zenye nguvu mbele za Mungu ndio
maana watu wengine wamekuwa na maombi ambayo hayana majibu.
Nikupe mfano huu, wazazi
wengi huwapatia watoto wao matakwa yao kulingana na hoja wanazokuja nazo kwa
wazazi wao kwa mfano jaribu kufikiri mzazi ambaye ana watoto wawili; mmoja
akaja kumuomba mzazi wake hela ili akanunue daftari na mwingine akaja kumuomba
mzazi wake hela ili akatembee pamoja na mrafiki zake, kati ya hawa watoto
wawili unahisi ni nani ambaye atajibiwa ombi lake kwa haraka?
Hoja zenye nguvu maana
yake ni sababu zenye nguvu zinazomfanya Mungu akupe kile ambacho unakiomba
kwake.
Kuna namna ya kibiblia ya
kutengeneza hoja zenye nguvu ili unapokwenda mbele za Mungu kuomba hoja zako
ziwe na nguvu na hatimaye Mungu ajibu maombi yako.
1.Mjue
Mungu
Watu wengi wanajikuta
wakiwa hawana majibu ya maombi sababu mojawapo ni kutomjua Mungu. Nataka
nikuonyeshe jambo lililofanya maombi ya Musa yakapata kibali mbele za Mungu
(Kutoka 32:7-14)
Kilikuwa ni kipindi
ambacho wana wa Israeli waliabudu ndama na kwa kufanya hivyo hasira ya Bwana
ikawaka juu yao na Bwana akataka kuwaangamiza, lakini Musa alikwenda mbele za
Mungu na hoja yenye nguvu(sababu iliyomfanya Mungu aghairi alichokuwa amekusudia
kukifanaya) kwa kuwa Musa alimjua Mungu ni Mungu ashikaye maagano kutokana na
hilo Musa alimwambia Mungu “Kwa nini wamisri waseme kuwa Mungu aliwatoa Misri
ili apate kuwaangamiza” na pia Musa akamwambia Mungu “kumbuka uliahidi kuwa
utauzidisha uzao wa Ibrahimu ili uwe kama mchanga wa Bahari sasa kwa nini
uwaangamize hawa watu?”, Mungu aliposikia hoja hiyo ya Musa, Mungu alighairi
kuwaangamiza kwa kuwa kuna hoja yenye nguvu ililetwa na Musa na ikasababisha
Mungu aghairi alichokuwa amekikusudia, Mungu alighairi kuwaangamiza si kwa
sababu waliomba msamaha ila ni kwa sababu Musa alijua kuwa Mungu anashika
maagano na kwa kuwa aliahidi kuwa atauzidihsa uzao wa Ibrahimu ndio maana Musa
alikwenda mbele za Mungu kwa ujasiri na hoja yake ikawa na nguvu mbele za Bwana.
Ni vema unapokwenda mbele
za Mungu kuomba uwe na ufahamu juu ya kile ambacho Mungu ameahidi juu ya hicho
unachotaka kuomba kwa kuwa Mungu analiangalia neno lake ili apate kulitimiza (Yeremia
1:12) ndio maana Musa alimwambia Mungu akumbuke kile alichomuahidi
Ibrahimu na Isaka na Yakobo juu ya uzao wao na Mungu aliposikia alijibu yale
maombi kwa haraka sana.
2.Mkumbushe
Mungu (Ahadi zake au mambo mema uliyotenda)
(Kutoka 32:7-14)
Wakati ambapo Mungu
ametaka kuwaangamiza wana wa Israeli kutokana na kuabudu ndama, Musa
alimkumbusha Mungu kuhusu alichowahidi Ibrahimu na Isaka na Yakobo, Mungu
aliposikia kuhusu hilo ghafla akaamua kughairi kile alichokuwa amekusudia
kuwatenda.
(Isaya 38:1-8)
Mfalme Hezekia alipougua
na akawa kwenye hatari ya kufa alikwenda mbele za Mungu kuomba, hoja yake
ilikuwa na nguvu kwa kuwa alimkumbusha Mungu juu ya mambo ambayo aliyatenda
katika taifa alililiongoza, Mungu aliposikia hoja hiyo ghafla akamwambia
Hezekia kuwa amemsikia na amemuongezea miaka kumi na mitano.
Unapokuwa na jambo la
kumkumbusha Mungu hilo jambo linaifanya hoja yako unayopeleka mbele za Mungu
inakuwa na nguvu na Mungu anakuwa tayari kujibu maombi yako?
Unapotenda jambo jema
unajiweka ukumbusho mbele za Bwana (Matendo ya Mitume 9:36-41) unapotoa
sadaka zako unajiwekea ukumbusho mbele za Bwana (Matendo ya Mitume 10;1-4) na
kwa kuwa Mungu huwa ana kitabu cha ukumbusho (Malaki 3;16) unapomkumbusha
Bwana kuhusu uliyotenda hoja hiyo inakuwa na nguvu mbele za Bwana na Mungu
hawezi kukuacha jinsi ulivyo.
1 Maoni
Asante nimejifunza sana. Mungu akubariki
JibuFuta