Shetani aliweka wazo ndani ya moyo wa Yuda mtoto wa Mzee Iskariote ili amsaliti Bwana Yesu Kristo, rejea Yohana 13:1-3.
Nimekutazamisha hilo ili kukufundisha kuwa mbinu mojawapo ya vita vya kiroho ni kuwaombea wengine, JIZOEZE KUWAOMBEA WENGINE.
Kemea kila roho inayotumia mioyo ya watu wengine kama vituo vya kukushambulia kwa njia ya kukupa mawazo mabaya, ushauri mbaya, kukutia hofu nakadhalika.
Angusha kila wazo au mawazo yaliyomo ndani ya mioyo ya watu wengine ambayo yamewekwa na Shetani ili kukuharibu, kukuharibia mambo mbalimbali na kukuangamiza (2 Wakorintho 10:4-5.
Muombe Mungu ashughulikie watu ambao mioyo yao imebeba vitu vya kishetani dhidi yako nakadhalika.
NB: Ninayo mengi ya kukuandikia ila zingatia hayo, wakati unajiombea usisahau kuwaombea wengine kwa kuwa wakati mwingine shetani hufanya vita na wewe kutokea kwenye mioyo ya watu wengine, wakati mwingine huwezi kujua shetani anatumia moyo wa nani kukabiliana na wewe.

0 Maoni