NZI ALIYENITAFAKARISHA MAMBO MENGI


 Sikumoja nikiwa mahali fulani nimetulia peke yangu nikanunua maziwa kwenye duka lililokuwa jirani.

Nilipofungua maziwa ili ninywe akaja nzi akatua juu ya mfuniko wa yale maziwa, nilielewa lengo la nzi yule ni kulamba maziwa yaliyokuwa kwenye mfuniko.

Nzi yule hakuniogopa, hakufikiri kama naweza kumuua, hakufikiri tukio lile lingeweza kuwa sababu ya kupoteza uhai wake. Tukio la yule nzi lilinitafakarisha sana.

Nina mambo mengi ya kukufundisha kupitia tukio la nzi yule;

1. Kuna wakati unapotaka kufanikisha malengo yako ISHINDE HOFU KWANZA, yule nzi angetawaliwa na hofu asingeweza kulamba maziwa. Fahamu kuwa kuna vitu haujapata, kuna viwango haujafika kwa sababu ya HOFU TU ILIYO NDANI YAKO.

2. Shetani ni kama yule nzi, akipata nafasi anaua, anaharibu, anaiba. Kumbuka kuwa nzi huweza kusababisha magonjwa mbalimbali kutokana na uchafu anaobeba.

Chapisha Maoni

0 Maoni