KUJAA ROHO MTAKATIFU - Seh ya 2


KUJAZWA ROHO AU KUJAA ROHO MTAKATIFU MAANA YAKE NINI? 

Kujaa Roho Mtakatifu ni pale Roho Mtakatifu anapochukua nafasi yote katika moyo wa mtu au ni pale Roho Mtatifu anapochukua udhibiti wa moyo wote wa mtu. Kwa hiyo ukisikia neno kujaa Roho Mtakatifu unapaswa kufahamu kuwa ni pale Roho Mtakatifu amechukua nafasi yote kwenye moyo wako au ni pale Roho Mtakatifu anapochukua udhibiti wote wa moyo wako.

Ni kama ndoo ya maji ikiwa tupu au ikiwa na maji kidogo, ukiijaza maji yakajaa kunakuwa hakuna nafasi ya kuweka maji mengine, hivyo ndivyo lilivyo suala la kujaa Roho Mtakatifu, ndoo ikijaa maji halafu ukazidi kuongeza maji, yale maji yatabubujika au yatafurika. Roho Mtakatifu akijaa sana ndani ya moyo wa mtu linatokea jambo linaitwa bubujiko.

(Matendo ya Mitume 5:1-10)

Anania alidanganya kuhusu mauzo ya kiwanja ambacho aliahidi akiuza atatoa pesa yote ya mauzo ili iwasaidie wakristo wenzake lakini alipouza hakuleta pesa yote ya mauzo.

Mtume Petro alimuuliza hivi "kwa nini shetani amekujaza moyo wako? maana yake ni kwamba shetani alichukua udhibiti wa moyo wa Anania, Mtume Petro aliita jambo hilo "ujazo wa shetani au kujaa kwa shetani kwenye moyo wa Anania" ndio maana aliuliza kwa nini shetani amekujaza moyo wako.

Nimekuonyesha mfano huo ili kuhusianisha na ujazo wa Roho Mtakatifu, kujaa Roho Mtakatifu ni pale Roho Mtakatifu anachukua nafasi yote kwenye moyo wa mtu, ni pale Roho Mtakatifu anachukua udhibiti wote wa moyo wa mtu, ni pale Roho Mtakatifu amejaa kwenye moyo wa mtu.


👉👉👉👉 Fuatilia sehemu ya tatu

Chapisha Maoni

0 Maoni