KUJAA ROHO MTAKATIFU - Seh ya 1


 (Waefeso 5:18)

Nitafundisha yafuatayo (Yaliyomo)

1. Kujaa Roho Mtakatifu ni nini au kujazwa Roho Mtakatifu ni nini

2. Jinsi ya kuwa mtu uliyejaa Roho Mtakatifu kila wakati

UTANGULIZI

Watu wengi wamekuwa wanapata mkanganyiko wa kiufahamu kuhusu suala la kujazwa Roho Mtakatifu au kujaa Roho Mtakatifu, wengine hudhani kuwa kunena kwa lugha ndio kujazwa Roho Mtakatifu na mengineyo yanayofanana na hayo.

Unachopaswa kufahamu ni kwamba kujaa Roho Mtakatifu au kujazwa Roho Mtakatifu ni jambo tofauti na kunena kwa lugha ndio maana si kila aliyejaa Roho Mtakatifu hunena kwa lugha. 

Biblia inaeleza mambo mbalimbali kuhusu kunena kwa lugha, baadhi ni haya yafuatayo;-

1. Kunena kwa lugha ni udhihirisho mmojawapo unaoonyesha mtu amepokea ujazo wa Roho Mtakatifu (Matendo ya mitume 2:1-4).

2. Kunena kwa lugha ni ishara mojawapo inayomtambulisha mwamini (mtu aliyemwamini Yesu), rejea (Marko 16:17).

3. Kunena kwa lugha ni kitendo cha roho yako kuwezeshwa na Roho Mtakatifu kusema siri zako kwa Mungu bila watu wengine kusikia unachomwambia Mungu (1 Wakorintho 14:2).

3. Kunena kwa lugha ni kitendo cha Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu kuijenga nafsi yake (1 Wakorintho 14:4).

Msisitizo: Kujaa Roho Mtakatifu ni jambo lingine na kunena kwa lugha ni jambo lingine - si kila aliyejaa Roho hunena kwa lugha.

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Fuatilia sehemu ya pili nitafundisha kuhusu kujaa Roho Mtakatifu ni nini hasa.

Chapisha Maoni

0 Maoni